33. Allaah atawazungumzisha waja wake wote pasina mkalimani

Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

watu watamuona Allah (´Azza wa Jall) kwa macho yaliyo vichwani mwao nay eye atawahesabu bila ya kuwepo pazia wala mkalimani.

MAELEZO

Kwa nini amesema “siku ya Qiyaamah”? Kwa sababu (Jall wa ´Alaa) haonekani hapa duniani.

Kwa macho yaliyo vichwani mwao huku ni kukanusha tafiri mbovu za wale wanaosema:

“… watamuona.”

maana yake ni kwa nyoyo zao na si kwa macho yao.

Siku ya Qiyaamah wakati wa hesabu mja atakuwa faragha na Mola Wake na Allaah atamfanyia hesabu na hakutokuwepo mkalimani. Mkalimani ni yule anayetarjumu kutoka lugha moja kwenda nyingine kama ambaye anatarjumu maana kutoka lugha ya kingereza kwenda lugha ya kiarabu au kinyume chake. Huyu ndiye anaitwa “mkalimani.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 75
  • Imechapishwa: 05/02/2018