18- Kufa juu ya kitendo chema. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kusema “Laa ilaaha illa Allaah” hali ya kuwa ni mwenye kutafuta uso wa Allaah kisha akamalizia hilo basi ataingia Peponi, yule mwenye kufunga siku moja hali ya kuwa ni mwenye kutafuta uso wa Allaah kisha akamalizia hilo basi ataingia Peponi na yule mwenye kutoa swadaqah yoyote hali ya kuwa ni mwenye kutafuta uso wa Allaah kisha akamalizia hilo basi ataingia Peponi.”

Ameipokea Ahmad (05/391) kutoka kwa Hudhayfah ambaye amesema:

“Nimemuegemeza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kifuani mwangu akasema:

“Yule mwenye kusema “Laa ilaaha illa Allaah” hali ya kuwa ni mwenye kutafuta uso wa Allaah… “

Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. al-Mundhiriy (02/61) amesema:

“Haina neno.”

al-Haafidhw bin Hajar amesema katika “al-Fath” (06/43) alipokuwa anataja sababu za kufa shahidi na sifa zake:

“Tumekusanyikiwa kutoka katika njia zilizo nzuri zaidi ya sifa ishirini.”

Tanbihi

al-Bukhaariy ameweka mlango katika “as-Swahiyh” yake (06/89): “Mlango unaozungumzia mtu kutosema: “Fulani ni shahidi”. Watu wengi wanachukulia wepesi jambo hili. Wanasema: “Shahidi fulani,  shahidi fulani… “

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 58-59
  • Imechapishwa: 13/02/2020