33. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa sita wa al-Baqarah


al-´Ayyaashiy amesema wakati alipokuwa akifasiri Aayah:

وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ

“[kumbuka] Alipojaribiwa Ibraahiym na Mola wake kwa maneno [maamrisho], naye akayatimiza.” (02:124)

“Aliyatimiza kupitia Muhammad, ´Aliy na maimamu kutoka katika kizazi cha ´Aliy waliyotajwa kwenye Kauli ya Allaah:

ذُرِّيَّةً بَعْضُهَا مِن بَعْضٍ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

“Vizazi wao kwa wao, na Allaah ni Mwenye kusikia yote daima, Mjuzi wa yote daima.” (03:34)

Allaah Amesema:

لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ

“Haiwafikii ahadi Yangu madhalimu.”

Ibraahiym alisema: “Ee Mola Wangu! Je, kizazi changu kitakuwa na madhalimu?” Akasema: “Ndio, fulani, fulani na fulani na wale wenye kuwafuata.” Hivyo Ibraahiym akasema: “Ee Mola Wangu! Waharakishie yale uliyomuahidi Muhammad na ´Aliy. Waharakishie nusura Yako.” Hayo ndio Aliyoashiria pale Aliposema:

وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ ۚ وَلَقَدِ اصْطَفَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ

“Na nani atakayejitenga na imani ya Ibraahiym isipokuwa anayeitia nafsi yake upumbavu? Na kwa yakini Tumemteua duniani, naye Aakhirah ni miongoni mwa [waja] wema.” (02:130)

Imani maana yake ni uongozi… Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُ إِلَىٰ عَذَابِ النَّارِ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ

“Na atakayekufuru, Nitamstarehesha kidogo kisha Nitamsukumiza katika adhabu ya Moto – na ni pabaya paliyoje pahala pa kuishia!”. (02:126)

Ibraahiym akasema: “Ee Mola Wangu! Ni kina nani hao Utakaowastarehesha?” Akasema: “Ni wale waliokanusha ujumbe Wangu; fulani, fulani na fulani.”[1]

Ametakasika Allaah! Tokea wakati wa Ibraahiym tayari fikira za Raafidhwah zilikuwa zimeshaanza kutajwa na kutangazwa. Maamrisho ambayo Ibraahiym alitimiza ilikuwa ni ´Aliy na maimamu kutoka kwenye kizazi chake na sio ´Aqiydah, matendo na mambo mengine yaliyowekwa kwenye Shari´ah?

Madhalimu ni fulani, fulani, fulani na wale wenye kuwafuata. Bi maana Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na maimamu wa Uislamu katika Maswahabah na wale waliowafuata kwa wema. Dhuluma zao tayari zilikuwa zimeshatajwa tokea wakati wa Ibraahiym!?!? Ilihali Raafidhwah, na khaswa Baatwiniyyah, wao ndio watu wema kabisa na wasiopendelea… Ni upetukaji mipaka wa sampuli gani! Ni shirki ya sampuli gani! Ni uongo wa sampuli gani!

Ibraahiym hakuna mwingine aliyemjali isipokuwa ´Aliy peke yake na yale Allaah Aliyomuahidi na Kumnusuru Kwake kwa ajili ya Raafidhwah!?!? Usidanganyike na kutajwa kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hiyo ni sitara tu wanayoitumia kufunika upotevu wao.

Imani ya Ibraahiym ambayo baada yake ilifuatwa na Manabii, Mitume na vitabu haihusiani na kitu kingine isipokuwa uongozi ambao Raafidhwah wanaamini na sio dini iliyokamcka ilio na Tawhiyd, kupambana na shirki, upotevu na ukhurafi!?!?

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/57).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 68
  • Imechapishwa: 19/03/2017