32. Waumini watamuona Mola wao siku ya Qiyaamah pasi na kizuizi


Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

17- Kuamini Muonekano siku ya Qiyaamah. Watamuona Allaah (´Azza wa Jall) kwa macho yaliyo vichwani mwao na yeye atawafanyia hesabu pasi na pazia wala mkalimani.

MAELEZO

Miongoni mwa mambo ya ´Aqiydah muhimu tena makubwa ni kuthibitisha kuonekana kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Waumini watamuona Mola Wao siku ya Qiyaamah kwa macho yao kama wanavyouona mwezi usiku wa mwezi mng´aro na kama wanavyoliona jua waziwazi pasi na mawingu – kama ilivyokuja katika Hadiyth Swahiyh. Kumepokelewa Hadiyth nyingi zinazothibitisha waumini kumuona Mola Wao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 72
  • Imechapishwa: 27/01/2018