32. Unasemaje kwa mwenye kusema kuwa ummah wa leo wa Kiislamu haupo?

Swali 32: Unasemaje kwa mwenye kusema kuwa ummah wa leo wa Kiislamu haupo?

Jibu: Kusema kuwa ummah wa Kiislamu haupo ni jambo linapelekea kuikufurisha miji ya Kiislamu yote[1]. Maneno haya maana yake ni kwamba hakuna miji ya Kiislamu. Yanakwenda kinyume na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hatokuacha kuwepo kikundi kutoka katika ummah wangu hali ya kuwa ni chenye kushinda juu ya haki. Hakitodhurika na wale wenye kuwakosesha nusura wala wale wenye kwenda kinyume nao mpaka ifike amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) wakiwa katika hali hiyo.”[2]

Haijalishi kutakuwa na upotofu na ukafiri kiasi gani ni lazima kubaki kundi hili la Kiislamu.

Hakuna jambo la kukosekana ummah wa Kiislamu na himdi zote njema anastahiki Allaah. Si sharti jamii ya Kiislamu, kundi hili lililonusuriwa, liwe limesalimika na madhambi. Kwa sababu maasi madhambi yalipatikana hata wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakati wa makhaliyfah wake, lakini walikuwa wakikabiliana nayo na kuyakemea.

[1] Kwa masikitiko makubwa kuna ambaye anajinasibisha na ulinganizi na ambaye anaitwa kuwa eti ni kiongozi wa mwamko alisema hivyo. Kuna kipindi fulani alitoa muhadhara at-Twaaif kwa jina “al-Ummah al-Ghaa-ibah”, Ummah usiokuwepo.

[2] Muslim (3/1037).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 89-90
  • Imechapishwa: 31/05/2023
  • mkusanyaji: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy