32. Radd kwa wanaokanusha Allaah kuwa na mikono

Kuhusu wakanushaji ambao wanakanusha mikono miwili ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) – kama ambavyo vilevile wanakanusha sifa zingine zote – wanaipindisha maana mikono ya kwamba maana yake ni uwezo au kwamba maana yake ni neema. Wanasema kuwa mikono ya Allaah maana yake ni uwezo. Wanafasiri maneno Yake (Ta´ala):

لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

“Niliyemuumba kwa mikono Yangu.” (38:75)

kwamba maana yake ni uwezo Wangu. Tunawaraddi kwa kuwaambia: Allaah (´Azza wa Jall) ameitaja mikono kwa njia ya uwili. Je, Allaah (Jalla wa ´Alaa) ana nguvu mbili au ana nguvu moja? Jibu ni kuwa Allaah ana nguvu moja. Si sawa kusema kwamba Allaah ana nguvu mbili. Maneno Yake:

لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

“… Niliyemuumba kwa mikono Yangu.”

Je, mtu anawea kusema:

“Niliyemuumba kwa nguvu zangu mbili.”?

Hakuna hata mmoja aliyesema hivi.

Kuhusu kuipindisha kwao kwamba maana yake ni neema. Wanasema ni kama mfano wa mtu kusema “wewe una mkono kwangu” akikusudia “wewe una neema kwangu”. Hivyo wanafasiri:

لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

“… Niliyemuumba kwa mikono Yangu.”

kwamba maana yake ni neema zangu mbili. Tunawaraddi kwa kusema: Je, Allaah (Jalla wa ´Alaa) hana isipokuwa neema mbili peke yake au uhakika wa mambo ni kuwa neema zote zinarejea Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala)?

Jengine ni kuwa mikono miwili ya Allaah ikifasiriwa kuwa ni nguvu  na uwezo kutakuwa hakuna tofauti kati ya Aadam na viumbe wengine. Itakuwa Allaah ameumba viumbe wote kwa nguvu na uwezo Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Hivyo Aadam (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) atakuwa hana tofauti na wengine. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amempambanua aliposema:

لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ

“… Niliyemuumba kwa mikono Yangu.”

Hivi ndivyo wanavyoraddiwa watu hawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 92-93
  • Imechapishwa: 09/01/2024