32. Mume anatakiwa kumtendea mke wema


Miongoni mwa haki za mke juu ya mume wake ni yeye kumtunza kwa wema kwa njia zote ambazo kwa mujibu wa ada inachukuliwa kuwa ni wema. Hata hivyo kwa sharti matunzo hayo yawe hayaenda kinyume na Shari´ah ya Mola wa walimwengu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Haki za wanawake juu yenu ni nyinyi kuwatendea wema.”[1]

[1] at-Tirmidhiy (1163), an-Nasaaiy (9123) na Ibn Maajah (1851). Nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa at-Tirmidhiy.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 47
  • Imechapishwa: 24/03/2017