5- Asiyeweza kufunga kushindwa kwa kuendelea ambako hakutarajiwi kuondoka kama mfano wa mtumzima na mgonjwa mwenye ugonjwa usiyotarajiwa kupona kama mfano wa mgonjwa wa kansa na mfano wake. Mtu kama huyu si lazima kwake kufunga kwa sababu hana uwezo. Allaah (Subhaanah) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

”Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[2]

Lakini ni lazima kwake badala ya kufunga kutoa chakula kwa kumlisha maskini kwa kila siku moja. Kwa sababu Allaah amefanya kulisha chakula kulingana na swawm wakati ambapo mtu alikuwa na chaguo kufanya moja kati ya mawili hayo mara ya kwanza ilipofaradhishwa swawm. Kwa hiyo ikalazimika jambo hilo liwe ndio badali ya swawm wakati wa mtu kushindwa kwa sababu linalingana  nayo.

Yuko na chaguo kati ya kuwatenganisha ambapo kila maskini mmoja akampa Mudd ya ngano, robo pishi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Mudd ambayo ni sawa na nusu kilo na gramu kumi kwa mchele mzuri. Chaguo lingine pia anaweza kutengeneza chakula na akawaita maskini kwa kiasi cha siku anazodaiwa. al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kuhusu mzee mtumzima asipoweza kufunga basi itambulike kuwa Anas alitoa chakula baada ya kuwa mtumzima kwa mwaka mmoja au miaka miwili ambapo kila siku alimlisha akiwapa mkate na nyama ambapo akafungua.”

Ibn ´Abbaas (Rahimahumaa Allaah) amesema kuhusu mzee mtumzima, mwanamke mtumzima ambao hawawezi kufunga kwamba watapaswa kumlisha maskini kwa kila siku moja iliyowapita. Mapokezi hayo yamepokelewa na al-Bukhaariy.

[1] 64:16

[2] 02:286

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 45-46
  • Imechapishwa: 25/04/2020