32. Dalili ya thelathini kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

30- Muhammad ametukhabarisha: Hamad ametuhadithia: Sulaymaan ametuhadithia: al-Miqdaam bin Daawuud ametuhadithia: ´Aliy bin Ma´bad ametuhadithia: Wahb bin Raashid ametuhadithia, kutoka kwa Farqad, kutoka kwa Anas ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) alimteremshia ufunuo Mtume mmoja katika Mitume yake: “Inakuweje waja Wangu wanaingia katika Nyumba yangu – yaani misikiti – kwa nyoyo zisizokuwa safi na mikono michafu? Wanadanganyika Nami? Wanataka kunihadaa Mimi? Naapa kwa ufalme Wangu, utukufu Wangu na ujuu katika ujuu Wangu ya kwamba nitawajaribu kwa jaribio ambalo nitamfanya mvumilivu kuwa ni mwenye kudangana. Hakuna yeyote katika wao atakayesalimika isipokuwa yule aliyeomba kama du´aa ya mwenye kuzama.”[1]

[1] Abu Nu´aym al-Aswbahaaniy amesema:

”Hadiyth za Wahb na Farqad si hoja kwa yale waliyopwekeka katika kuyasimulia.” (Hilyat-ul-Awliyaa’ (3/56))

adh-Dhahabiy amesema:

“Si Swahiyh, lakini ni yenye kuwezekana.” (al-´Uluww, uk. 52)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 118-119
  • Imechapishwa: 10/06/2018