32. Dalili ya kwamba Mtume alimuona Mola wake kwa macho yake katika safari ya usiku mbinguni

32- Yahyaa bin ´Ammaar al-Imaam ametuhadithia: Muhammad bin al-Fadhwl (Muhammad bin Ishaaq bin Khuzaymah) ametuhadithia: ´Umar bin Hafsw ash-Shaybaaniy ametuhadithia: Mansuur bin Ismaa´iyl al-Hanafiy ametuhadithia: Babu yangu Mansuur bin ´Abdillaah amenihadithia: Muhammad bin Sahl bin Hamduuyah ametuhadithia: Mahmuud bin Aadam ametuhadithia… ح Muhammad bin Mahmuud ametuhadithia: an-Nu´aym ametuhadithia: Haatim bin Mahbuub ametuhadithia… ح Imaam Yahyaa ametuhadithia: Muhammad bin al-Fadhwl bin Muhammad bin Ishaaq bin Khuzaymah ametuhadithia: Babu yangu ametuhadithia: ´Abdul-Jabbaar bin al-A´laa´ ametuhadithia: Ibn Khuzaymah amesema: Sa´iyd bin ´Abdir-Rahmaan al-Makhzuumiy ametuhadithia: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa ´Ikrimah: Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema kuhusiana na:

وَمَا جَعَلْنَا الرُّؤْيَا الَّتِي أَرَيْنَاكَ إِلَّا فِتْنَةً لِّلنَّاسِ

“Hatukuijaalia ndoto ambayo tulikuonyesha isipokuwa ni mtihani kwa watu.”[1]

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona kwa macho Yake usiku aliyosafirishwa.”[2]

Matamshi ni ya ´Abdul-Jabbaar. ´Umar bin Hafsw ameongeza:

“Haikuwa maono ya usingizini.”[3]

[1] 17:60

[2] al-Bukhaariy (6613).

[3] ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy amesema:

”Mwandishi anaonelea kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona Mola wake kwa macho yake katika hali ya kuwa macho pindi alipopandishwa mbinguni katika safari ya usiku. Hata hivyo Maswahabah walitofautiana katika masuala haya. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) anathibitisha kuonekana. Wakati huo huo kuna mapokezi kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) yanayokanusha kuonekana kwa macho. Amesema:

”Atakayesema mambo matatu basi amemzulia Allaah uongo mkubwa… mwenye kusema kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona Mola wake amemzulia Allaah uongo mkubwa.”

Mapokezi yake yote yanapatikana katika al-Bukhaariy na Muslim.

Amethibitisha vilevile ya kwamba yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya Aayah:

مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ

”Moyo haukukadhibisha yale aliyoyaona.” (53:11)

وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ

”Hakika amemuona katika uteremko mwingine.” (53:13)

na akasema:

”Mimi ndiye wa kwanza katika Ummah kumuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya hilo na akasema: ”Huyo alikuwa ni Jibriyl. Sikumuona katika umbile lake la asli isipokuwa mara mbili hizi.”

Hakupinga kuonekana kutokana na ufahamu na ijitihadi yake, isipokuwa ni kutokana na maneno yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ibn Mas´uud alikuwa na maoni hayo hayo kama ´Aaishah.

Kwa vile maoni haya yapo katika al-Bukhaariy na Muslim, Ibn Hajar ametaja maoni ya wale wanaothibitisha na maoni ya wale wanaopinga. Halafu akabainisha ya kwamba mapokezi kutoka kwa Ibn ´Abbaas yametajwa sehemu yake hali ya kuyafungamanisha na moyo, na hali ya kutofungamanishwa. Kisha akasema ni lazima kuyafasiri yale ambayo hayakufungamanishwa kwa yale yaliyofungamanishwa. Baada ya hapo akaoanisha maoni ya ´Aaishah yanayokanusha na maoni ya Ibn ´Abbaas yanayothibitisha na hivyo inakuwa kukanusha kwake kunahusiana na kuonekana kwa macho na kuthibitisha kwake [Ibn ´Abbaas] kunahusiana na kuonekana kwa moyo. Halafu akasema:

”Kumuona kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa moyo hakukusudiwi elimu peke yake, kwa kuwa yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa daima ni mjuzi juu ya Allaah.” (Fath-ul-Baariy (08/608))

Kuoanisha kwake ni kuzuri na kwa njia hiyo yatachukuliwa mapokezi yote.

Kuhusu yale yaliyonakiliwa kutoka kwa Imaam Ahmad ya kwamba anathibitisha kuonekana kwa macho, Ibn-ul-Qayyim amepinga upokezi huo na kusema kuwa ulitumiwa vibaya na mmoja katika wapokezi.” (Tazama ”Zaad-ul-Ma´aad” (01/59)) (al-Arba´uun fiy Dalaa´il-ut-Tawhiyd, uk. 81-82)

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 63
  • Imechapishwa: 07/02/2017