32. Dalili juu ya mkono wa Allaah 17


31- al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Yuusuf bin Muusa ametuhadithia: Abu ´Abdir-Rahmaan al-Muqriy ametuhadithia: Hayaawah bin Shurayh ametuhadithia: Abu Haani´ ametuhadithia ya kwamba amemsikia Abu ´Abdir-Rahmaan al-Hubliy akisema kuwa amemsikia ´Abdullaah bin ´Amr akisema kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Nyoyo za wanaadamu zote ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa huruma, kama vile moyo mmoja; anazigeuza vile Atakavyo.” Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Allaah, ambaye unazigeuza nyoyo! Zigeuze nyoyo zetu katika utiifu Wako.”[1]

[1] Muslim (2654), Ahmad (2/168) na an-Nasaa’iy (7739).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 71
  • Imechapishwa: 01/03/2018