17-  Kufa hali ya kuwa katika mawindo doriani katika njia ya Allaah. Kuhusu hilo tutataja Hadiyth mbili:

A- “Lindo la mchana na usiku ni bora kuliko kufunga mwezi na kusimama usiku kuswali. Kama atakufa basi yataendelea matendo yake aliyokuwa akiyafanya, atapitishiwa riziki yake na ataaminishwa kutokamana na watoaji mitihani wawili.”

Ameipokea Muslim (06/51), an-Nasaa´iy (02/63), at-Tirmidhiy (03/18), al-Haakim (02/80), Ahmad (05/440 na 441) kutoka katika Hadiyth ya Salmaan al-Faarisiy. Ameipokea at-Twabaraaniy (6179) na amezidisha:

“… na atafufuliwa siku ya Qiyaamah akiwa ni shahidi.”

Lakini katika cheni ya wapokezi wake wapo ambao hawajulikani na al-Haythamiy katika “al-Mujma´” (05/290) na al-Mundhiriy ameinyamazia katika “Targhiyb” (02/150).

B- “Kila maiti hukhitimishwa juu ya matendo yake isipokuwa yule aliyekufa hali ya kulinda katika njia ya Allaah. Hakika yeye anakuziwa matendo yake mpaka siku ya Qiyaamah na huaminishwa na mtihani wa kaburi.”

Ameipokea Abu Daawuud (01/391), at-Tirmidhiy (03/02) na ameifanya kuwa ni nzuri. Vilevile imepokelewa na al-Haakim (02/144), Ahmad (06/20) kutoka katika Fadhwaalah bin ´Ubayd. al-Haakim amesema:

“Ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 58
  • Imechapishwa: 11/02/2020