123- Kusherehekea kwa Ka´bah kuvishwa pazia.

124- Kusherehekea kwa sehemu ya kusimama Ibraahiym kuvishwa pazia.

125- Kufunga vitambara sehemu ya kusimama Ibraahiym na mimbari ili kuweza kufikia haja mbalimbali.

126- Mahujaji kuandika majina yao kwenye nguzo na kuta za Ka´bah na kuambizana kufanya hivo.

127- Kuonelea kufaa kupita mbele ya mwenye kuswali katika msikiti Mtakatifu na kufanya upinzani na yule mswaliji ambaye anawazuia.

128- Kumwita yule ambaye amekwishahiji “al-Hajj”.

129- Kutoka Makkah kwa ajili ya kufanya ´Umrah ya kujitolea/ya sunnah.

130- Kutoka msikiti Mtakatifu kinyumenyume baada ya kumaliza kufanya Twawaaf-ul-Wadaa´.

131- Kuipaka rangi nyumba ya mwenye kuhiji kwa rangi nyeupe, kuchora picha na kuandika jina lake na tarehe ni lini kafanya hajj.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 55
  • Imechapishwa: 22/07/2018