31. Uwajibu wa kuitikia mwaliko

29- Ni wajibu kwa yule mwenye kualikwa katika walima basi aitikie wito. Kuna Hadiyth mbili juu ya hilo zifuatazo:

1- Mwacheni huru aliye mikononi mwa maadui, itikie mwaliko na watembeleeni wagonjwa.”[1]

2- Atapoalikwa mmoja wenu katika karamu ya ndoa basi aitikie. Ni mamoja ikiwa ni karamu ya harusi au nyengineyo. Yule ambaye hakuitikia wito basi amemuasi Allaah na Mtume Wake.”[2]

[1] Ameipokea al-Bukhaariy (09/198), ´Abd bin Humayd katika “al-Muntakhab min Musnad” (01/65) kupitia Hadiyth ya Abu Muusa al-Ash´ariy.

[2] Ameipokea al-Bukhaariy (09/198), Muslim (04/152), Ahmad (6337), al-Bayhaqiy (07/262) kupitia Hadiyth ya Ibn ´Amr.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 154
  • Imechapishwa: 21/03/2018