31. Qur-aan imeanza kwa Allaah


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kwake ndiko imeanza na Kwake ndiko itarudi na kwamba amezungumza kwayo kihakika

MAELEZO

Kwake ndiko imeanza – Bi maana imeteremshwa kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa sababu Allaah amezungumza kwayo kihakika na Jibriyl akasikia kutoka Kwake na akamteremshia nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baadaye Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawafikishia Ummah wake. Kwa hiyo ni maneno ya Allaah kikweli na sio kimafumbo. Kuhusu maneno Yake:

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ

“Hakika hii bila shaka ni kauli ya mjumbe mtukufu, mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa anayemiliki ‘Arshi.”[1]

Bi maana Jibriyl (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maneno Yake:

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تُؤْمِنُونَ

“Hakika hii bila shaka ni kauli ya Mtume mtukufu, na si kauli ya mshairi; ni machache mno yale mnayoamini.”[2]

Bi maaan Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mara ameyaegemeza kwa mjumbe wa kimtu, mara nyingine ameyaegemeza kwa mjumbe wa ki-Malaika na wakati mwingine ameyaegemeza kwa nafsi Yake (Ta´ala).

Jibu mtu anatakiwa kusema kwamba maneno yanaegemezwa kwa yule aliyeanza kuyasema. Kuhusu kuyaegemeza kwa Jibriyl au kwa Muhammad ni uegemezwaji wa ufikishaji. Haiwezekani kabisa neno moja likasemwa na wasemaji wengi. Ni dalili inayofahamisha kuwa ni maneno ya Allaah. Lakini ameyaegemeza kwa Jibriyl na kwa Muhammad pale aliposema:

إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ

“Hakika hii bila shaka ni kauli ya Mtume mtukufu.”

uegemezaji wa ufikishaji. Maneno huegemezwa kwa yule aliyeanza kuyasema na si kwa yule aliyeyasema hali ya kuyafikisha na kuyatekeleza. Hili ndio jibu ya shubuha hii waliyoishikilia.

[1] 81:19-20

[2] 69:40-41

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 52
  • Imechapishwa: 16/03/2021