31. Mwenye kuacha swalah amekufuru


Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Yule mwenye kuacha swalah amekufuru. Hakuna katika matendo kitu kukiacha ni kufuru isipokuwa swalah. Mwenye kuiacha ni kafiri. Allaah amehalalisha kumuua.”

MAELEZO

Waandishi wa “as-Sunnah” wamepokea kwa cheni ya wapokezi Swahiyh ya kwamba Buraydah bin al-Haaswib (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”[1]

Muslim amepokea kwamba Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kati ya mtu na ukafiri ni kuacha swalah.”[2]

Abu Waa-il bin Shaqiyq bin Salamah amesema:

“Hakuna kitu ambacho Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakiona kukiacha ni ukafiri isipokuwa swalah.”[3]

Hapa Ahmad anasema:

“Hakuna katika matendo kitu kukiacha ni kufuru isipokuwa swalah. Mwenye kuiacha ni kafiri. Allaah amehalalisha kumuua.”

[1] at-Tirmidhiy (2621), an-Nasaa’iy (463) na Ibn Maajah (1079). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

[2] at-Tirmidhiy (2619), an-Nasaa’iy (464) na Ibn Maajah (1078). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

[3] at-Tirmidhiy (2622). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 131-132
  • Imechapishwa: 25/04/2019