31. Mume anatakiwa kumhudumia mke

Miongoni mwa haki za mke juu ya mume wake ni yeye kumhudumia kutokana na ada ilivo. Wakati anapokula na yeye pia amlishe. Wakati anapovaa na yeye pia amvishe. Kinachotakikana kwa mwanaume ni yeye kumhudumia mke na kumruzuku kutokana na ada ilivo, bila ya israfu wala ubakhili. Asifanye ubakhili kwa kile alonacho na kutompa. Atangamane naye kutokana na ada ilivo. Kama jinsi hatakiwi vilevile kumpa zaidi ya uwezo wake na zaidi ya ada inavosema. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Haki zao juu yenu ni nyinyi kuwapa matumizi na kuwavisha kwa wema.”[1]

[1] Muslim (1218).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 46-47