31. Msingi wa kumi: Kulazimiana na Qur-aan na Sunnah katika hali zote

10- Kulazimiana kwetu na Qur-aan na Sunnah katika kazi na hali zetu zote

Kulazimiana kwetu na Qur-aan na Sunnah katika kazi na hali zetu zote ndio msingi mkubwa zaidi na wenye kuihukumu. Hayo ni kutokana na maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا

“Haiwi kwa muumini mwanamme na wala kwa muumini mwanamke pindi Allaah anapohukumu na Mtume Wake jambo lolote iwe wana khiyari katika jambo lao – na yule anayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi kwa hakika amepotoka upotofu wa wazi.”[1]

إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَخْشَ اللَّـهَ وَيَتَّقْهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ

“Hakika si vyenginevyo kauli ya waumini wa kweli wanapoitwa kwa Allaah na Mtume Wake ili awahakumu kati yao husema: “Tumesikia na tumetii” – na hakika hao ndio wenye kufaulu; na yeyote yule atakayemtii Allaah na Mtume Wake na akamkhofu Allaah na akamcha, basi hao ndio wenye kufuzu.”

mpaka aliposema:

قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْهِ مَا حُمِّلَ وَعَلَيْكُم مَّا حُمِّلْتُمْ ۖ وَإِن تُطِيعُوهُ تَهْتَدُوا ۚ وَمَا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ

”Sema: Mtiini Allaah na mtiini Mtume. Mkikengeukia mbali, basi hakika jukumu lake ni lile alilobebeshwa tu nanyi ni juu yenu yale mliyobebeshwa. Na mkimtii mtaongoka; na hakuna juu ya Mtume isipokuwa kufikisha kwa wazi.”[2]

Zipo Aayah nyingi zinazohimiza juu ya Qur-aan na Sunnah na amri ya kushikamana navyo. Vivyo hivyo Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Miongoni mwa hayo ni yale yaliyothibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika hijah ya kuaga (ambayo ndio kulikuwa mkusanyiko mkubwa wa waislamu):

“Hakika nimekuachieni kile ambacho hamtopotea baada yangu endapo mtashikamana nacho barabara; Kitabu cha Allaah.”[3]

Imethibiti pia katika “Mustadrak” ya al-Haakim ambaye amepokea kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimekuacheni vitu viwili ambavyo hamtopotea iwapo mtashikamana navyo barabara. Havitotengana mpaka nitapojiwa kwenye Hodhi.”[4]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema kuhusu maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى

”Basi atakayefuata uongofu Wangu hatopotea na wala kutaabika.”[5]

 “Allaah (´Azza wa Jall) amemdhamini yule ambaye atasoma Qur-aan na akayafuata yale yaliyomo ndani yake kwamba hatopotea duniani na wala hatotaabika huko Aakhirah.”[6]

[1] 33:36

[2] 24:51-54

[3] Muslim (1218).

[4] al-Haakim (01/172) (319). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (5248).

[5] 20:123

[6] Ibn Jariyr katika ”Tafsiyr” yake (18/389).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 75-76
  • Imechapishwa: 17/11/2020