31. Msafara wa Quraysh unasamilika dhidi ya waislamu

Kuhusu Basbas bin ´Amr al-Juhaniy na ´Adiy bin Abiyz-Zaghbaa´ al-Juhaniy wao walifika katika maji ya Badr na wakamsikia kijakazi akimwambia mwenzake: “Hutolipa deni langu?” Yule mwenzake akajibu: “Msafara utafika kesho au kesho kutwa. Nitaufanyia kazi kisha ndio nikulipe deni lako.”

Majdiy bin ´Amr akayathibitisha maneno yake. Pindi wanaume wote wawili waliposikia maneno ya yule kijakazi wakaondoka zao na Abu Sufyaan akiwa nyuma yao. Akamuuliza Majdiy bin ´Amr: “Hukumuona yeyote katika Maswahabah wa Muhammad?” Akasema: “Hapana, isipokuwa wapandaji wawili waliotua katika kilima kile.” Abu Sufyaan akaenda mahala pao. Akachukua kinyesi za ngamia na akakuta mbegu za tende ambapo akasema: “Hii ni lishe ya Yathrib!” Akauchukua msafara na kuupitisha njia ya pwani na akawa amesalimika. Akatuma ujumbe kwa Quraysh kuwafahamisha kwamba amesalimika na kuwaamrisha warudi nyuma. Quraysh wakapata khabari hizo ambapo Abu Jahl akakataa na kusema: “Ninaapa kwa Allaah haturudi mpaka tufike kwenye maji ya Badr. Tutakuwa huko kwa siku tatu na tutakunywa pombe na waimbaji wanawake wadumbwize juu ya vichwa vyetu ngoma ili siku zote tuwe ni wenye kushinda adabu/heshima kwa waarabu.  al-Akhnas bin Shurayq akarudi na kabila lake lote la Banuu Zuhrah na kusema: “Mmeenda kwa ajili ya kuokoa msafara wenu – na tayari umeshasalimika.”

Hakuna yeyote kutoka katika Banuu Zuhrah aliyepigana isipokuwa tu maami wawili wa Muslim bin ´Ubaydillaah bin ´Abdillaah bin Shihaab bin ´Abdillaah az-Zuhriy. Wao ndio walishiriki katika Badr na wakauawa wakiwa ni makafiri.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 48-49
  • Imechapishwa: 04/05/2018