31. Kitabu kinatakiwa kugawanywa milango

Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Nitayagawanya yale niliyokuahidi mlango kwa mlango ili yawe rahisi kwa mwanafunzi kuyafahamu – Allaah (Ta´ala) akitaka. Yeye pekee Ndiye tunamtaka tawfiki na Yeye pekee Ndiye tunamtaka msaada. Hapana nguvu wala namna isipokuwa kwa msaada wa Allaah, Aliye juu kabisa, Aliye mtukufu. Swalah na amani zimwendee bwana wetu na Mtume Wake Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

MAELEZO

Anamzungumzisha mwalimu wake ambaye kamwomba kutunga kijitabu hiki na utangulizi wake wenye manufaa.

Ametaja kwamba amekigawanya kitabu katika milango ili iweze kumsaidia mwanafunzi na msomaji kuelewa hatua kwa hatua. Vinginevyo inakuwa vigumu kwa msomaji kukisoma kitabu ambacho hakina milango.

Kisha akamwomba Allaah tawfiki na msaada. Amejiweka mbali kutokamana na nguvu na namna na akamnasibishia nayo Allaah (´Azza wa Jall). Akamalizia kumwomba Allaah amswalie na kumsalimu Mtume Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 29
  • Imechapishwa: 25/07/2021