31. Dalili ya kwamba Allaah hushuka katika mbingu ya dunia

31- Muhammad bin Muusaa as-Swayrafiy ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdillaah as-Swaffaar ametuhadithia: Ibn Abiyd-Dunyaa ametuhadithia: al-Qaasim bin Hishaam ametuhadithia: Abuu Mishar ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Abdillaah bin Ismaa´iyl ametuhadithia: al-Awzaa´iy ametuhadithia: Yahyaa bin Abiy Kathiyr amenihadithia: Hilaal bin Abiy Maymuunah amenihadithia: ´Atwaa´ bin Yasaar amenihadithia: Rifaa´ bin ´Araabah al-Juhaniy (Radhiya Allaahu ´anh) amenihadithia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kunapopita nusu ya usiku – au alisema “Kunapopita theluthi ya usiku” – Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika ile mbingu ya chini ya dunia na kusema: “Simuulizi yeyote juu ya waja Wangu isipokuwa Mimi Mwenyewe; ni nani aniombaye nimuitikie? Ni nani aniombaye msamaha nimghufurie?” mpaka kupambazuke.”[1]

[1] Ahmad (4/16), an-Nasaa’iy (6/122-123) Ibn Maajah (1367), ad-Daaraqutwniy katika ”an-Nuzuul” (67), ad-Daarimiy (1489), Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 132, na al-Aajurriy katika ”ash-Shariy´ah”, uk. 310-311.

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 61
  • Imechapishwa: 07/02/2017