31. Dalili juu ya mkono wa Allaah 16


30- al-Hasan bin ´Aliy al-Baswriy ametuhadithia: Abur-Rabiy´ az-Zahraaniy ametuhadithia: Abu Ma´mar ametuhadithia: ´Awn bin ´Abdillaah bin al-Haarith ametuhadithia, kutoka kwa kaka yake, kutoka kwa baba yake ´Abdullaah bin al-Haarith bin Nawfal aliyeeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) ameumba vitu vitatu kwa mkono Wake. Amemuumba Aadam kwa mkono Wake. Ameiandika Tawraat kwa mkono Wake na ameipanda Firdaws kwa mkono Wake.”[1]

[1] al-Bayhaqiy amesema:

“Kuna Swahabah anayekosekana katika mlolongo wa wapokezi, Mursal.” (al-Asmaa´ was-Swifaat (2/125))

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 69-71
  • Imechapishwa: 28/02/2018