114- Kupuuzilia mbali kile kichinjwa cha wajibu na badala yake kutoa thamani yake kuwapa masikini. Baadhi wanafanya hivi kwa kudai kwamba nyama yake inaenda chini ya udongo kutokana na wingi wake na hakuna wanaofaidika nayo isipokuwa wachache tu[1].

115- Baadhi yao kuchinja kichinjwa cha Tamattu´ Makkah kabla ya siku ya Nahr.

116- Kuanza kunyoa upande wa kushoto kwenye kichwa cha yule mnyolewaji.

117- Kunyoa tu sehemu ya robo ya kichwa.

118- al-Ghazaaliy amesema katika “al-Ihyaa´”:

“Sunnah ni kuelekea Qiblah wakati wa kunyoa.”

119- Kuomba du´aa wakati wa kunyoa kwa kusema:

الحمد لله على ما هدانا وأنعم علينا اللهم هذه ناصيتي بيدك فتقبل مني

“Himdi zote anastahiki Allaah kwa yale Aliyotuongoza na akatuneemesha. Ee Allaah! Uendeshaji wangu uko mikononi Mwako. Hivyo nikubalie… “

120- Kufanya Twawaaf kwenye misikiti ilio karibu na mahali pa kurusha mawe.

121- Kuona kuwa imependekezwa kuswali swalah ya ´Iyd Minaa siku ya Nahr.

122- Mwenye kufanya hajj ya Tamattu´ kuacha kufanya Sa´y baada ya Twawaaf-ul-Ifaadhwah.

[1] Hii ni miongoni mwa Bid´ah mbaya kabisa kwa sababu ina maana ya kuiteketeza Shari´ah kwa sababu tu ya maoni. Isitoshe ni kwamba mahujaji wenyewe ndio wenye jukumu la kama kichinjwa kitaleta faida au hakitoleta. Kwa sababu hawashikamani na yale maelekezo ya Shari´ah yenye hekima, kama ilivyobainishwa katika “asili”, uk. 87-88.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 54-55
  • Imechapishwa: 22/07/2018