15 na 16- Kufa katika njia ya kutetea dini na nafsi. Katika hilo zipo Hadiyth mbili:

A- “Mwenye kuuawa kwa sababu ya kutetea mali yake ni shahidi, mwenye kuuawa kwa sababu ya kumtetea mke wake ni shahidi, mwenye kuuawa kwa sababu ya kuitetea dini yake ni shahidi na mwenye kuuawa kwa sababu ya kutetea damu yake ni shahidi.”

Ameipokea Abu Daawuud (02/275), an-Nasaa´iy na at-Tirmidhiy (02/316) na ameifanya kuwa Swahiyh, Ahmad (1652 na 1653) kutoka kwa Sa´iyd bin Zayd. Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.

B- “Mwenye kuuawa kwa sababu ya kutetea kitu chake kinachotaka kudhulumiwa.”

Ameipokea an-Nasaa´iy (02/173-174) kupitia kwa Suwayd bin Muqarrin na Ahmad (2780) kupitia kwa Ibn ´Abbaas. Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh ikiwa imesalimika na kukatika baina ya Sa´d bin Ibraahiym Ibn ´Abdir-Rahmaan bin ´Awf na kati ya Ibn ´Abbaas. al-´Alaa´ amenakili katika “Jaamiy´ at-Tahswiyl”, uk. 180 kutoka Ibn Madiyniy ya kwamba hakumsikia Swahabah yeyote. Lakini njia moja wapo inaitia nguvu nyingine. Katika njia ya kwanza hakuna aliyemfanya kuwa ni mwaminifu isipokuwa tu na Ibn Hibban.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 57
  • Imechapishwa: 11/02/2020