31. al-Qummiy upotoshaji wa tano wa al-Baqarah


al-´Ayyaashiy amesema pinid alipokuwa akifasiri Aayah:

وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ لَا تَسْفِكُونَ دِمَاءَكُمْ وَلَا تُخْرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَارِكُمْ ثُمَّ أَقْرَرْتُمْ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ

“Na [kumbukeni] Tulipochukua fungamano lenu [Tukawaambia]: “Msimwage damu zenu, wala msitoe nafsi zenu kutoka miji yenu;” kisha mkakubali nanyi mnashuhudia.” (02:84)

“Aayah hii haikuteremshwa katika mnasaba mwingine isipokuwa ni kwa mnasaba wa Abu Dharr na ´Uthmaan. Sababu ya kuteremshwa ´Uthmaan aliamrisha Abu Dharr afukuzwe kwenda Rabdhah. Abu Dharr, ambaye alikuwa ni mtu mgonjwa na anatembea na fimbo, akaenda kwa ´Uthmaan ambaye mbele yake alikuwa na dirhamu 100.000. Zimeletwa kutoka pande mbali mbali. Marafiki zake wamemzunguka na huku wanatarajia atawagawanyia nazo. Abu Dharr akamwambia ´Uthmaan: “Hizi ni pesa gani?” Akasema: “Ni dirhamu 100.000 zimeletwa kwangu kutoka pande mbali mbali. Nataka kuweka kiasi mfano wake kisha nimpe tuzo langu.” Abu Dharr akasema: “Ee ´Uthmaan! Ziko wapi zingine? Dirhamu 100.000 au ni dinari nne?” Akasema: “Ni dirhamu 100.000… “[1]

Ametakasika Allaah! Je, Aayah hii imeteremka katika mnasaba wa Abu Dharr wakati wa ukhalifah wa ´Uthmaan baada ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameshakufa? Baada ya miaka 24 Hijrah? Ni Mtume yupi aliyeteremshiwa Qur-aan hii? Mtu huyu alikuwa ni bingwa namna gani wa Qur-aaan, sababu ya kuteremshwa kwa Aayah na wakati wake!?!? Raafidhwah ni wajinga kiasi gani!!! Ni wepesi ulioje kwao kumsemea uongo Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Qur-aan!!!

[1] Tafsiyr al-Qummiy (1/51).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 63-64
  • Imechapishwa: 19/03/2017