30. Wazushi wa leo wanajificha nyuma ya ´Aqiydah ya Khawaarij

Swali 30: Je, mwenye kujificha na mwenye kudhihirisha maasi na mtu wa Bid´ah wote wawili wanaraddiwa sawa au kwa kila mmoja ana namna yake na kutegemea na yale aliyomo?

Jibu: Ambaye anajificha na mwenye kudhihirisha, haya ni kuhusu maasi. Lakini mtu wa Bid´ah anaona yuko katika haki na kwamba anafanya lililo jema. Yeye siku zote anakuwa mwenye kufanya waziwazi. Kunakuwepo ambaye anamsapoti mzushi huyu kwa njia isiyokuwa ya Kishari´ah. Huyu ndiye ambaye anatakiwa kusimamiwa kidete na kubainisha jambo lake. Wazushi wa leo wanajificha nyuma ya ´Aqiydah ya Khawaarij na wanawadhihirishia watu kuwa hawaonelei hivo. Ni waongo.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017