Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

26- Amewaumba viumbe kwa ujuzi Wake.

MAELEZO

Amesema (Subhaanah):

أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ

“Kwani hajui Yule aliyeumba na hali Yeye ni Mwenye kuendesha mambo kwa upole, Mwenye khabari zote?”[1]?

Uumbaji Wake (Ta´ala) ni dalili juu ya ujuzi na uwezo Wake, kama alivosema:

وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعْجِزَهُ مِن شَيْءٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا

“Hakuna chochote kimshindacho Allaah mbinguni na wala ardhini, hakika Yeye ni Mjuzi wa yote, Mweza wa yote.”[2]

[1] 67:14

[2] 35:44

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 47
  • Imechapishwa: 24/09/2019