30. Qur-aan ni maneno ya Allaah na haikuumbwa – hii ndio I´tiqaad ya wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah

Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

Hivyo ndivyo alivyosema Maalik bin Anas, Ahmad bin Hanbal na Fuqahaa´ kabla yao na baada yao.  Na kujadiliana juu yake ni kufuru.

MAELEZO

Haya ndio maoni ya maimamu. Miongoni mwao akiwemo Maalik ambaye alikuwa ni mwanachuoni wa al-Madiynah. Kuhusu Imaam Ahmad aliadhibiwa juu ya hili na akaudhiwa (Rahimahu Allaah). Pamoja na hivyo akawa na subira. Kadhalika ni maoni ya maimamu wengine wa Ahl-us-Sunnah. Haya ndio maoni yao.

Si kwamba ni Imaam Ahmad na Maalik ndio walisema maoni haya peke yao. Maoni haya yalisemwa na waliokuwa kabla yao katika Maswahabah, Taabi´uun, waliofuata baada ya Taabi´uun na maimamu waliokuja baada yao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 70
  • Imechapishwa: 27/01/2018