30. Mwanadamu kamwe habaki hali ya kuwa si mwenye kufanya kazi

Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameufaradhishia moyo matendo ya kuamini na viungo vya mwili matendo mema ya kufanya.

MAELEZO

Allaah ameufaradhishia ulimi adhkaar zilizowekwa katika Shari´ah na usomaji wa Qur-aan. Haya ni matendo ya ulimi.

Pia ameufaradhishia moyo matendo. Moyo pia una matendo; kumcha Allaah, kumpenda, kumtegemea Yeye, kurejea Kwake. Haya ni baadhi ya matendo ya moyo.

Vilevile amevifaradhishia viungo vya mwili matendo. Ni matendo yenye kuonekana waziwazi kama mfano wa Rukuu´, Sujuud na kupambana katika njia ya Allaah.

Matendo ya moyo ndio ile ´Aqiydah; kumwamini Allaah, khofu, tisho, shauku, woga, matarajio, mapenzi na mengineyo.

Shaykh (Rahimahu Allaah) hakutaja matendo ya ulimi kwa sababu yanaingia katika matendo ya viungo vya mwili. Kwa sababu ulimi ni kiungo miongoni mwa viungo.

Mtendaji analipwa thawabu au kuadhibiwa kutegemea na matendo yake. Mtu akitafakari basi ataona kuwa ni mwenye kushughulika ima kwa uinje au kwa undani. Kamwe habaki hali ya kuwa si mwenye kufanya kazi. Siku moja matendo yake yatamrudilia yeye mwenyewe; kama yalikuwa ni mema, basi atalipwa thawabu, na kama yalikuwa ni maovu, basi ataadhibiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 14/07/2021