30. Mtume anapata khabari ya idadi ya Quraysh katika Badr


Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakachukia kutokana na waliyosikia. Walitamani lau wangelikuwa upande wa msafara wa Abu Sufyaan na wakawa karibu ili waweze kuuvamia. Kwa sababu kulikuwa kuna wepesi kuliko kupambana na kundi la Quraysh lililokuwa na nguvu sana na lililokuwa limejiandaa. Wakaanza kuwapiga. Wanapopatwa na maumivu wanasema: “Sisi ni watu wa Abu Sufyaan.” Wanapowaacha wanasema: “Sisi ni kutoka Quraysh.” Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomaliza kuswali akasema: “Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake kwamba mtawapiga mkiwa wakweli na mkawaacha waseme uongo.” Kisha akasema kuwaambia wawili wale: “Nambieni Quraysh wako wapi?” Wakasema: “Wako nyuma ya dune lile.” Akawauliza: “Ni wangapi?” Wakajibu: “Hatujui.” Akawauliza: “Huchinja kiasi gani kwa siku?” Wakasema: “Mara kumi, mara tisa.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ni kati ya watu 900 mpaka 1000.”[1]

[1] Ahmad (1/117). Swahiyh kwa mujibu wa al-Arnaa’uut.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 04/05/2018