Ni lazima kwa yule mwenye kuchelea juu ya nafsi yake kuharibika na upotevu alazimiane na kufuata mfumo huu. Naapa kwa Allaah kwamba Salaf walijizuia na kusimama kwa elimu. Haafidhw bin ´Asaakir amesema katika “Taariykh Dimashq” kuhusu wasifu wa Ahmad bin ´Awnillaah ambaye alikuwa mmoja katika wanachuoni wa Sunnah akiwa ni mwenye kunukuu kutoka kwa Abu ´Abdillaah Muhammad bin Ahmad bin Mufarrij:

“Abu Ja´far Ahmad bin ´Awnillaah akiwafuatilia Ahl-ul-Bid´ah, wakali juu yao, akiwadhalilisha, akifuatilia makosa yao, akienda mbio kwelikweli kuwadhuru, akiwakanyaga kwelikweli, akimakinika juu yao basi anawashambulia ipasavyo na hawabakizi. Kila aliyekuwa katika wao alikuwa ni mwenye kumuogopa na akijichunga naye. Hampaki mafuta yeyote katika wao kwa hali yoyote wala hawapi amani. Akipata uovu kutoka kwa mmoja wao na kukatolewa ushahidi mbele yake kwamba mtu huyo amepinda kutokamana na Sunnah, basi anamtupulia mbali na kumfedhehesha. Baada ya hapo anatangaza utajo wake na watu wajitenge mbali naye. Pindi watu wanapokufanyika kwa mnasaba wa sherehe basi anamuibisha kwa kumtaja kwa ubaya na anamsakama kwelikweli mpaka anamwangamiza au anamwondosha kutoka katika madhehebu yake mabaya na ´Aqiydah yake mbovu. Aliendelea na mwenendo huu hali ya kuwa ni mwenye kupambana kwa ajili ya kutafuta uso wa Allaah mpala pale alipokutana na Allaah (´Azza wa Jall). Anayo misimamo inayotambulika na inayotajwa dhidi ya wakanamungu.”[1]

[1] Taariykh Madiynati Dimashq (05/118).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 17/11/2020