177- Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kamwe hakukuwa mkate wa shayiri kwa familia ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[1]

178- Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaweza kushinda nyusiku nyingi za kufuatana akiwa na njaa na familia yake haina chakula cha jioni. Mara nyingi walikuwa wakila mkate wa shayiri.”[2]

179- Kulisemwa kuambiwa Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh):

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikula mkate mweupe?” Akasema: “Sikumuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akila mkate mweupe mpaka alipokutana na Allaah (´Azza wa Jall).”[3]

180- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakula wakashiba mkate wa ngano nyusiku tatu za kufuatana tangu alipofika al-Madiynah mpaka alipofariki.”[4]

181- ´Urwah bin az-Zubayr amesema:

“Shangazi yangu alinambia: “Ee mwangu! Ninaapa kwa Allaah tulikuwa tunaweza kumaliza nyusiku arubaini na nyumbani kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakukongwi moto na wala hakuashwi taa.” Nikamuuliza: “Mlikuwa mnaishi kwa kitu gani?” Akasema: “Viwili vyeusi; tende na maji na hakuna kingine.”[5]

182- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Kitanda cha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kilikuwa kimetengenezwa kwa ngozi iliyoshinikizwa makuti.”[6]

[1] at-Tirmidhiy (2464) ambaye amesema: ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

[2] at-Tirmidhiy (2465), Ibn Maajah (3347) na Ahmad (1/255). at-Tirmidhiy amesema: ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

[3] at-Tirmidhiy (2469) na Ibn Maajah (3335). at-Tirmidhiy amesema: ”Hadiyth ni Swahiyh.”

[4] al-Bukhaariy (8/121) na Muslim (18/105).

[5] al-Bukhaariy (8/121) na Muslim (18/107).

[6] al-Bukhaariy (8/121) na Muslim (14/58).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 112-115
  • Imechapishwa: 18/03/2017