Mnyonyeshaji na mjamzito ni lazima kwao kulipa siku nyingine zile siku walizokula. Ambaye amekula kwa kukhofia afya ya mtoto wake – mbali na kulipa – ni lazima vilevile kulisha masikini juu ya kila siku aliyokula. ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ibn ´Abbaas na Maswahabah wengineo wametoa fatwa kuhusu mjamzito na myonyeshaji pindi watapochelea juu ya watoto wao wale na walishe chakula masikini juu ya kila siku.”[1]

Bi maana walipe na walishe chakula kwa kila siku moja.

[1] Zaad-ul-Ma´aad (02/29).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/392)
  • Imechapishwa: 30/05/2021