30- Muhammad bin Muusaa as-Swayrafiy ametuhadithia: al-Asamm ametuhadithia: Haaruun bin Sulaymaan ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Mahdiy ametuhadithia, kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abuu Swaalih, kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) amesema: “Mimi niko vile mja Wangu anavyonidhania. Mimi niko pamoja naye pale anaponiomba. Akinikaribia shibiri moja, basi Mimi namkaribia dhiraa moja. Akinikaribia dhiraa moja, basi Mimi namkaribia pima. Akinijia kwa kutembea, basi Mimi namwendea kwa kuchapuka.”[1]

[1] al-Bukhaariy (7405) na Muslim (2675).

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 60
  • Imechapishwa: 05/02/2017