30. Dalili ya kumi na saba kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

31- Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waumini watakusanyika siku ya Qiyaamah wakiwa ni wenye wasiwasi na waseme: “Lau tutashufai mbele ya Mola wetu ili atusalimishe kutokamana na sehemu yetu hii.” Hivyo waende kwa Aadam na waseme: “Ee Aadam! Wewe ni baba wa watu. Allaah amekuumba kwa mkono Wake na akawaamrisha Malaika wakusujudie… “[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim ambaye pia ameipokea kupitia kwa Abu Hurayrah.

[1] al-Bukhaariy (8/160) na Muslim (194).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 27
  • Imechapishwa: 02/07/2019