30. Dalili ya ishirini na nane kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

28- Nilimsomea Abul-´Abbaas Ahmad bin al-Mubaarak bin Sa´d: Babu yangu Abul-Ma´aaliy Thaabit bin Bundaar bin Ibraahiym amekukhabarisheni: Abu ´Aliy al-Hasan bin al-Husayn bin Duumaa ametuhadithia: Makhlad bin Ja´far ametuhadithia: Abu Muhammad al-Hasan bin ´Aliy al-Qattwaan ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Iysaa al-´Attwaar ametuhadithia: Ishaaq bin Bishr ametuhadithia: ´Uthmaan bin as-Saaj amenihadithia, kutoka kwa Muqaatil bin Hayyaan, kutoka kwa Abul-Jaruud al-´Abdiy, kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah ambaye amesema:

“Nilifikiwa na khabari ya Hadiyth kuhusu kisasi na mpokezi wake alikuwa Misri. Nikanunua ngamia na kusafiri kwenda kwake. Nilisafiri mwezi mzima kabla ya kufika Misri. Nikaulizia kuhusu mpokezi wa Hadiyth hiyo ambapo nikaelekezwa kwake. Nikakuta mlango wake umefungwa na kuna kijana mweusi. Nikasema: “Bwana wako yuko hapa?”Hakujibu kitu. Kisha akaingia ndani na kumweleza bwana wake kwamba kuna mmbedui mmoja wa kiarabu yuko nje ya mlango. Akatoka nje na kusema: “Wewe ni nani?” Nikajibu: “Ni Jaabir bin ´Abdillaah.” Akasema: “Ingia ndani.”Nikaingia ndani na kusema: “Nimefikiwa na khabari kwamba unaelezea Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu kisasi. Mimi sijaisikia na hakuna mwingine zaidi yako aliyeihifadhi.” Akasema: “Ndio. Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Allaah atawafufua watu siku ya Qiyaamah wakiwa miguu peku, uchi na bila kutahiriwa. Halafu anadi, ilihali huku amesimama juu ya ´Arshi Yake, kwa sauti ya juu ambayo itasikiwa na aliye karibu na aliye mbali: “Mimi ndiye Mfalme. Hakuna dhuluma hii leo. Nitamwacha yule aliyedhulumiwa kulipiza kisasi kwa aliyemdhulumu ijapokuwa ni kofi tu au pigo la mkono. Nitamwacha yule mbuzi asiyekuwa na pembe kulipiza kisasi kwa yule mbuzi mwenye pembe. Nitaiuliza bakora ni kwa nini ilimkwaruza mwenzie na nitaliuliza jiwe ni kwa nini lilimpata mwenzie. Kwa hayo nimewatuma Mitume Wangu na nimeteremsha Vitabu Vyangu na kuhusu hayo Nilisema:

وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ

“Tutaweka mizani za uadilifu siku ya Qiyaamah – basi nafsi haitodhulumiwa kitu chochote – ijapo ikiwa uzito wa mbegu ya hardali Tutaileta; na inatosheleza Kwetu kuwa wenye kuhesabu.”[1]

[1] 21:47 adh-Dhahabiy amesema:

”Ishaaq bin Bishr ni dhaifu na ameharibika.” (Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (9/478))

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 112-113
  • Imechapishwa: 10/06/2018