106- Kuoga kabla ya kurusha mawe.

107- Kuyaosha mawe kabla ya kuyarusha.

108- Kusema “Subhaan Allaah” na mengineyo nafasi inayotakiwa kusema “Allaahu Akbar”.

109- Kuongeza baada ya Takbiyr kwa kusema:

رغما للشيطان وحزبه اللهم اجعل حجي مبرورا وسعيي مشكورا وذنبي مغفورا اللهم إيمانا بكتابك واتباعا لسنة نبيك

“Hii ni dhidi ya shaytwaan na kundi lake. Ee Allaah! Ijaalie kuwa ni hajj yenye kukubaliwa, jitihada zenye kulipwa na dhambi yenye kughufuriwa. Ee Allaah! Nayafanya haya kwa kuamini Kitabu Chako na kufuata Sunnah za Mtume Wako.”

110- Baadhi ya waliokuja nyuma wameona kuwa ni Sunnah kusema kila wakati mtu anaporusha jiwe:

بسم الله والله أكبر صدق الله وعده

“Kwa jina la Allaah. Allaah ni mkubwa. Allaah amesema kweli ahadi Yake.”

Mpaka mwishoni wanasema:

وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

“Ijapokuwa watachukia makafiri.”

111- Kulazimiana na mitindo maalum wakati wa kurusha mawe. Kama kwa mfano kuweka ncha ya kidole gumba cha mkono wake wa kulia katikati ya kidole cha shahada. Kisha mtu analiweka jiwe juu ya kidole gumba halafu unalifyatua. Wengine wanasema mtu anatakiwa kukunja kidole cha shahada mpaka kiishilie kwenye kidole gumba hadi yote hayo yaonekane kama herufi “P”.

112- Kufanya kikomo umbali wa baina ya yule mrushaji na kule anakolenga kwa dhiraa tano na zaidi.

113- Kurusha viatu na vyenginevyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 54
  • Imechapishwa: 22/07/2018