Kuna aina mbili za utoaji mimba:

1- Lengo la kuiporomosha mimba ni kutoa kile kipomoko. Ikiwa kile kipomoko kimeshapuliziwa roho, bila ya shaka yoyote ni haramu kwa kuwa ni kuiua nafsi iliyoharamishwa pasina haki. Kuiua nafsi iliyoharamishwa bila ya haki ni jambo lililoharamishwa kwa mujibu wa Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya waislamu.

Ikiwa kuporomosha mimba ni kabla ya kipomoko kupuliziwa roho, wanachuoni wametofautiana juu yake. Baadhi ya wanachuoni wamejuzisha hilo, wengine wameliharamisha, wengine wakajuzisha kabla ya haijakuwa damu iliyoganda, bi maana kabla ya kufikisha siku arubaini na wengine wakasema kuwa inajuzu midhali kipomoko hakijapata umbo la mwanaadamu.

Kauli ilio salama ni kuwa ni haramu kuporomosha mimba ikiwa hakuna haja ya kufanya hivo kama kwa mfano mama ni mgonjwa na hawezi kubeba mimba na mfano wa hayo. Katika hali hii itafaa kuporomosha mimba ikiwa kipomoko hakijakuwa na umbo la mwanaadamu na Allaah ndiye anajua zaidi.

2- Lengo la kuporomosha mimba sio kuharibu kile kipomoko. Ikiwa mwanamke anajaribu kutoa mimba karibu na muda wa kuzaa basi inajuzu maadamu hilo litakuwa halina madhara kwa mama na mtoto na wala hakuna operesheni yoyote inayohitajika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016