3. Ni zipi nguzo za kuamini majina na sifa za Allaah?

Swali 3: Ni zipi nguzo za imani ya kuamini majina ya Allaah na sifa Zake?

Jibu: Ni tatu:

1- Imani ya kuamini majina mazuri yote.

2- Imani ya kuamini yale yote ambayo yanaashiriwa na sifa.

3- Imani ya kuamini hukumu ya sifa na yale mambo yenye kufungamana nazo.

Tunaamini kuwa Allaah ni mjuzi na ana elimu kamilifu iliokizunguka kila kitu.

Tunaamini kuwa Allaah ni muweza na ana uwezo mkubwa kabisa ambao kwao anakiweza kila kitu.

Tunaamini kuwa Allaah ni mwenye huruma na ni mwenye kurehemu na kwamba ana huruma mpana ambao anamrehemu amtakaye.

Hali kadhalika inahusiana na majina mengine yote mazuri na sifa na yale yenye kufungamna nayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamm-ul-Muhimmaat, uk. 25
  • Imechapishwa: 25/03/2017