Nasabu hii tuliyotaja mpaka kwa ´Adnaan hakuna tofauti yoyote juu yake. Imethibiti kupitia njia mbali mbali na maafikiano. Tofauti imekuja kwa nasabu kabla ya ´Adnaan. Lakini hata hivyo watafiti wa nasabu na wanatheolojia wa kiyahudi na kinaswara wamekubaliana juu ya kwamba ´Adnaan ni mmoja katika wana wa Mtume Ismaa´iyl. Kwa mujibu wa maoni sahihi ya Maswahabah na Taabi´uun Ismaa´iyl ndiye aliyekuwa anataka kuchinjwa. Ismaa´iyl ni mwana wa Ibraahiym. Kuna maoni mbali mbali juu ya kwamba kuna mababa wangapi walioko kati yao.

Idadi kubwa iliotajwa ni mababa arubaini. Idadi ndogo iliotajwa ni mababa saba. Kuna waliosema ni tisa wakati wengine wamesema kuwa ni kumi na tano. Kisha pia wakatofautiana juu ya majini yao.

Baadhi ya Salaf na maimamu wamechukizwa kujinasibisha kwa yeyote kabla ya ´Adnaan. Imesemekana pia kuwa Imaam Maalik bin Anas al-Asbahiy (Rahimahu Allaah) pia alikuwa akichukizwa na hilo.

Imaam Abu ´Umar bin ´Abdil-Barr amesema katika kitabu ”al-Inbaah”:

”Maimamu kuhusiana na suala hili kutokamana na nasabu ya ´Adnaan: ´Adnaan alikuwa mwana wa Udud ambaye alikuwa ni mwana wa Muqawwim ambaye alikuwa ni mwana wa Naahuur ambaye alikuwa ni mwana wa Twayrah ambaye alikuwa ni mwana wa Ya´rab ambaye alikuwa ni mwana wa Yashjab ambaye alikuwa ni mwana wa Naabit ambaye alikuwa ni mwana wa Ismaa´iyl ambaye alikuwa ni mwana wa Ibraahiym ambaye alikuwa ni mwana wa Twaarih (ambaye ndiye Aazar) ambaye alikuwa ni mwana wa Naahuur ambaye alikuwa ni mwana wa Shaaruukh ambaye alikuwa ni mwana wa Raa´uu ambaye alikuwa ni mwana wa Faalikh ambaye alikuwa ni mwana wa ´Aybar ambaye alikuwa ni mwana wa Shaalikh ambaye alikuwa ni mwana wa Arfakhshadh ambaye alikuwa ni mwana wa Saam ambaye alikuwa ni mwana wa Nuuh ambaye alikuwa ni mwana wa Laamak ambaye alikuwa ni mwana wa Muttuushalakh ambaye alikuwa ni mwana wa Akhnuuk (ambaye kwa mujibu wa Manabii wa Allaah Idriys (´alayhis-Salaam) ndio Nabii wa kwanza kupewa unabii baada ya Aadam na Shiyth na ndio wa kwanza kuandika kwa kalamu – na Allaah ndiye anajua zaidi) ambaye alikuwa ni mwana wa Yard ambaye alikuwa ni mwana wa Mahlayl ambaye alikuwa ni mwana wa Qaynan ambaye alikuwa ni mwana wa Yaanush ambaye alikuwa ni mwana wa Shiyth ambaye alikuwa ni mwana wa Aadam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Hivi ndivyo alivyotaja nasabu mwandishi wa ”as-Siyrah an-Nabawiyyah” ambaye ni Muhammad bin Ishaaq bin Yasaar al-Madaniy na watafiti wengine wa nasabu. Abul-´Abbaas ´Abdullaah bin Muhammad an-Naashiy al-Mu´taziliy ameiandika kwenye shairi alipokuwa akimsifu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Imaam Abu ´Umar ameinukuu na kadhalika Shaykh wetu [al-Mizziy] kwenye ”at-Tahdhiyb” yake. Shairi hilo ni lenye kugonga na mwanzo wake:

Namsifu Mtume wa Allaah ili nipate sehemu ya makao matukufu

Namsifu mtu mwenye kuwashinda weney kusifiwa wote

kwa sifa zake zilizotajwa kwa mbali na kwa karibu

Kabilah zote za kiarabu ni zenye kukutana na yeye kupitia kwa ´Adnaan. Kwa ajili hii ndio maana Allaah (Ta´ala) amesema:

قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ

“Sikuombeni ujira wowote ule juu yake isipokuwa mapenzi kwa ajili ya ujamaa wa karibu.” (42:23)

”Hakukuwa kabila lolote la kiarabu isipokuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na jamaa.”Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio msomi wao. Muslim amepokea kwenye ”as-Swahiyh” yake kupitia kwa Waathilah bin al-Asqa´ (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah amechagua Kinaanah kutoka kwenye kizazi cha Ismaa´iyl. Kisha akachagua Quraysh kutoka kwa Kinaanah. Halafu akachagua Banuu Haashim kutoka kwa Quraysh. Kisha akanichagua mimi kutoka kwa Banuu Haashim.”

Kadhalika wana wa Israaiyl na Mitume wao na wengine wanakutana naye kwa Ibraahiym (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) ambaye dhuriya yake Allaah aliwapa utume na kitabu. Allaha (Subhaanah) aliwaambia wana wa Israaiyl kupitia kwa Muusa (´alayhis-Salaam):

17 MOLA akanambia: ”Wana haki kwa waliyoyasema. 18 Mtume nitamtoa kati yao katika ndugu zao, mmoja mwenye kufanana na wewe, na nitaweka maneno yangu mwenye mdomo wake, na atawaambia yote ninayomwamrisha. 19 Kukiwepo yeyote asiyesikiza maneno yangu, maneno anayoyazungumza kwa jina langu, nitamalizana naye.”[1]

Hakuna yeyote mkubwa aliyezaliwa kutoka kwenye kizazi cha Ismaa´iyl ambaye ni mkubwa zaidi kuliko Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali uhakika wa mambo ni kwamba hakuna mwanaadamu yeyote aliyekuwa mkubwa kuliko Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hatokuwepo mpaka siku ya Qiyaamah. Imesihi ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mimi ndio bwana wa wanaadamu na sio fakhari. Aadam na Mitume wengine wote baada yake watakuwa chini ya bendera yangu.”

Imesihi ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nitakuwa na cheo ambayo viumbe wote wataitamani akiwemo Ibraahiym.”

Inahusiana na cheo chenye kusifika ambacho Allaah (Ta´ala) alimuahidi. Cheo hicho inahusiana na uombezi mkubwa pindi atapowaombea viumbe wote ili Allaah awasalimishe na mahala pa kisimamo, kama jinsi ilivyopokelewa kupitia Hadiyth Swahiyh na kwa kina kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mama yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaitwa Aminah ambaye alikuwa ni binti Wahb ambaye ni mwana wa ´Abdu Manaaf ambaye alikuwa ni mwana wa Zuhrah ambaye ni mwana wa Kullaab ambaye alikuwa ni mwana wa Murrah.

[1] (Kumbukumbu (18:17-19))

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 13-15
  • Imechapishwa: 18/03/2017