Ndugu! Mkishajua haya mnaweza mkajiuliza kama inawezekana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafa na kuacha nyuma yake kitu katika dini ambacho kinakurubisha kwa Allaah na asikibainishe? Hata siku moja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha dini yote ima kwa maneno, matendo na kukubali na amefanya hivo kwa njia ya kuanza mwenyewe au kwa kujibu maswali. Wakati mwingine Allaah alikuwa anamtuma bedui kutoka kijijini mashambani kuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuuliza swali la kidini ambalo Maswahabah hawakuuliza. Walikuwa ni wenye kufurahi kuja kwa mbedui na kumuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baadhi ya maswali.

Kitu kinachofahamisha hilo ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuacha kitu nyuma yake ambacho watu wanakihitajia katika ´ibaadah zao, mu´amala na mambo ya maisha yao isipokuwa amekibainisha. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

“Leo Nimekukamilishieni dini yenu, nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu.”[1]

[1] 05:03

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ibdaa´ fiy Kamaal-ish-Shar´ wa Khatwar-il-Ibtidaa´, uk. 4-5
  • Imechapishwa: 23/10/2016