3. Mfano wa tatu kuonyesha kuwa Raafidhwah ni Baatwiniyyah

3- al-´Ayyaashiy (02/50) amesema:

“Jaabir ameeleza kuwa amemuuliza Abu Ja´faar kuhusiana na Kauli Yake (Ta´ala):

وَيُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ

“Na Allaah Anataka Athibitishe haki kwa Maneno Yake na Akate mizizi ya makafiri.” (08:07)

Abu Ja´far amesema:

وَيُرِيدُ اللَّـهُ

“Na Allaah Anataka…”

Tafsiri yake iliyojificha ni kwamba Allaah Anataka lakini bado hajafanya hivo.

أَن يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ

“Athibitishe haki kwa Maneno Yake…”

Bi maana Aithibitishe haki kwa watu wa familia ya Muhammad.

بِكَلِمَاتِه

“… kwa Maneno Yake…”

Tafsiri yake iliyojificha ni ´Aliy. Yeye ndiye neno la Allaah kwa tafsiri iliyojificha.

وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ

“… na Akate mizizi ya makafiri”.

Ni Banuu Umayyah. Ni makafiri. Allaah Akate mizizi yao.

لِيُحِقَّ الْحَقَّ

“… ili Athibitishe Haki…” (08:08)

Bi maana Aithibitishe haki kwa watu wa familia ya Muhamamd (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi al-Mahdiy anapojitokeza.

وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ

“… na Abatilishe uongo… “

Bi maana al-Mahdiy. Wakati atapojitokeza uongo wa Banuu Umayyah utadhahiri kuwa ni uongo. Hii ndio maana ya:

لِيُحِقَّ الْحَقَّ وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ

“Ili Athibitishe Haki na Abatilishe uongo japokuwa wahalifu watachukia.”

Mhakiki ameelekeza katika “al-Bihaar”, “al-Burhaan” na “Ithbaat-ul-Hudaa”.

Jaabir ameeleza kuwa alimuuliza Abu ´Abdillaah Ja´faar bin Muhammad kuhusu tafsiri iliyojificha ya Aayah:

وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ الْأَقْدَامَ

“Na Akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, ili Akusafisheni kwayo, na Akuondosheeni uchafu wa shaytwaan [wa rai ovu], ili Atie nguvu nyoyo zenu na Athibitishe kwayo miguu.” (08:11)

Amesema:

“Mbingu kwa tafsiri iliyojificha ina maana ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maji ni ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu). Allaah Amefanya ´Aliy kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio tafsiri ya:

لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ

“… ili Akutwaharisheni kwayo…”

Ni ´Aliy. Allaah Husafisha mioyo kwa wale walio upande wake.

وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ

“… na Akuondosheeni uchafu wa shaytwaan [wa rai ovu]…”

Aliyeko upande wa ´Aliy huondoshewa uchafu wa Shaytwaan na moyo wake hufanywa ukawa na nguvu.

وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ الْأَقْدَامَ

“… na ili Atie nguvu nyoyo zenu na Athibitishe kwayo miguu.”

Bi maana ´Aliy. Aliyeko upande wa ´Aliy Allaah Huutia nguvu moyo wake kwa kupitia ´Aliy na Kumfanya imara kwa upande wa ´Aliy.

Angalia uchafu huu uliojengwa juu ya mfumo wa Baatwiniyyah pale ambapo:

1- Maneno ya Allaah ambayo Huithibitisha haki kuwa haki na Kubatilisha uongo kuwa uongo wamefanya kuwa ni ´Aliy.

2- Mbingu ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mvua ni ´Aliy ambayo Allaah Huisafisha mioyo ya wafuasi wake kwayo.

Aayah hizi zinahusiana na vita vya Badr na jinsi Allaah Alivyolinyanyua neno Lake na Kuinusuru dini Yake na Mtume Wake na waumini kwa kupitia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr, ´Umar na wale kumi waliobashiriwa Pepo. Akafanya Maneno Yake yakashinda uongo. Allaah Ameeleza kuwa sababu ya ushindi ni pamoja na:

1- Mvua kutoka mbinguni iliyowasafisha.

2- Kuwaondoshea uchafu wa Shaytwaan.

3- Kuithibtisha miguu yao.

4- Akawateremsha Malaika kuwasaidia.

5- Akatia khofu kwenye mioyo ya makafiri.

Lakini Baatwniyyah hawataki jengine isipokuwa kupotosha Aayah za Kitabu cha Allaah na kuzitoa katika maana yake tukufu na kuu na kuzipeleka katika madhehebu yao ya Baatwiniyyah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 18/03/2017