Maendeleo ya tatu:

Maendeleo ya tatu ni matangazo yaliyotoka kwenye gazeti la al-Ikhwaan kuhusiana na tamthili ya mwanzilishi wa Cairo na chuo kikuu cha Azhar al-Mu´izz li Diynillaah al-Faatwimiy. Tamthili ilikuwa imeandikwa na ndugu yake damu na kiongozi wa jumla (Hasan al-Bannaa) ´Abdur-Rahmaan as-Saa´aatiy. Tamthili ilichezwa kwa fikira na kukusanya urembo wa sanaa kwa enzi ya dini kwa aina ya wimbo. Ilifanyika jumatano tarehe 01 mei 1946. Tamthili ilitolewa na Siraaj Muniyr na Ahmad ´Abdul-Qaadiyr alisimamia sauti.

Tunamwacha msomaji afikiri mwenyewe jinsi mishale hii miwili inavopiga kwenye ´Aqiydah. Mshale mwingine umepiga kwenye ´Aqiydah na tabia pindi kunapoanza kuchezwa maigizo kwenye baadhi ya vyuo vikuu vya Kiislamu. Wale wenye kujishughulisha na mambo hayo, bi maana tamthili zisizokuwa na maana zinazoua tabia, ni wapotevu na wakodishwaji. Tamthili hizi kupatikana kwake ni lazima zijengwe juu ya uongo na hadisi. Haijalishi kitu ni manufaa gani watu wapotevu wanasema yanapatikana kwenye tamthili hizi, siku zote huwa zina madhara.

Tulitarajia al-Ikhwaan al-Muslimuun watakuwa pamoja na sisi dhidi ya Bid´ah zenye kudhuru au angalau kwa uchache wasihusiki, sio wao tena ndio wenye kuita kwazo kwa maneno na matendo. Tumeraddi kwa kina na kwenye matukio mbali mbali hoja za wenye kusema ya kwamba tamthili hizi zina faida kwenye maeneo mengine.

Tukiweka mambo ya tamthili kando na kuiangalia tamthili iliyochaguliwa, basi tutaona jinsi chaguo la al-Ikhwaan al-Muslimuun ni lenye kustaajabisha kabisa. Ni vipi wanaweza kuonelea urembo wa dini unaonyeshwa na khabathi huyu ´Ubaydiy? Pamoja na kwamba wanajua jinsi alivyoihujumu dini na kuibadili na kuigeuza kutokana na matamanio na shahawa ili aiangamize kabisa na kutekeleza matakwa ya babu yake Ibn Sabaa´! Ilikuwa ni myahudi Ibn Sabaa´ ndio aliujeruhi Uislamu kwa kuleta fitina kati ya ´Aliy na Mu´aawiyah [fitina ambayo] Uislamu bado unateseka nayo mpaka hii leo. Matendo ya al-Mu´izz li Diynillaah al-Faatimiy na khalifah wake hayakuwa ni ya siri na yenye kufichikana. Historia na wanahistoria wamekutana nayo, waislamu na wengine, wameandika jinsi walivyoishambulia dini kwa njia ambayo wanastahiki kulaaniwa na Allaah, Malaika na watu wote.

  • Mhusika: Shaykh Ahmad Shaakir, Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Afiyfiy, Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Wakiyl, Shaykh Muhammad Khaliyl al-Harraas, Shaykh Muhammad Haamid al-Faqiy na wengineo.
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 10-13 Gazeti al-Hadiy an-Nabawiy (1365/6)
  • mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy