3 – ´Allaamah na Muhaddith Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

Shaykh al-Albaaniy aliulizwa swali lifuatalo katika kanda “Liqaa´ AbiylHasan al-Ma´ribiy[1] m´a al-Albaaniy”:

Kutokana na msimamo wa Mashaykh wawili, muheshimiwa Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy na Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy, katika kupambana kwao na Bid´ah na maneno yaliyopinda, wako baadhi ya vijana ambao wanawatilia mashaka Mashaykh hao wawili kama wako katika msitari wa ki-Salafiy?

Akajibu (Rahimahu Allaah):

“Sisi, bila shaka tunamhimidi Allaah (´Azza wa Jall) Kujaalia katika Da´wah hii njema, iliyosimama juu ya Qur-aan na Sunnah na kwa mfumo wa wema waliotangulia, kuwepo hii leo walinganizi wengi katika miji mbalimbali ya Kiislamu ambao wanatekeleza wajibu huu ulio kwa baadhi ya watu (Fardhw Kifaayah), faradhi ambayo wamekuwa wachache mno wenye kuitekeleza katika ulimwengu wa Kiislamu wa leo. Kwa hivyo kuwasema vibaya hawa Mashaykh wawili, Shaykh Rabiy´ na Shaykh Muqbil, wanaolingania katika Qur-aan na Sunnah kwa mujibu wa ufahamu wa wema waliotangulia na kuwapiga vita wale wanaokwenda kinyume na mfumo huu sahihi, ni kama mnavyojua nyote (kuhusiana na watu hawa wanaowaponda) ni mmoja ya watu wawili: ima ni mjinga au mtu anayefuata matamanio yake.

Mjinga kama nilivyotangulia kusema, anaweza kuongozwa kwa urahisi, kwa kuwa mtu aina hii hudhani ana kitu katika elimu. Ataogoke wakati atapobainishiwa elimu sahihi. Ama kuhusiana na mtu anayefuata matamanio yake, tunamuomba Allaah kinga kutokamana na shari yake. Tunamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ima Amuongoze au Auvunje mgongo wake.”

Kisha Shaykh (Rahimahu Allaah) akasema:

“Ninatumia fursa hii kwa kusema yale niliyoyaona kwenye vitabu vya Shaykh na Dr. Rabiy´ ni yenye faida. Sikumbuki kama niliona kosa lolote kwake na kutoka nje ya mfumo ambao tunakutanisha naye au ambao yeye anakutanisha na sisi.”

Amesema pia katika kanda “al-Muwaazanaat Bid´at-ul-´Aswr” baada ya kuzungumzia Bid´ah hii ya leo:

“Kwa mukhtasari ninasema: Hakika mbebaji wa haki wa bendera ya Jarh na Ta´diyl leo, ni ndugu yetu Dr. Rabiy´. Wale wanaomraddi hawafanyi hivo kwa elimu kabisa, kwa sababu elimu iko pamoja naye. Pamoja na kwamba huwa ninasema kila siku, na humwambia maneno haya mara nyingi kwenye simu, ya kwamba lau angelikuwa mlaini katika usulubu wake, basi ingelikuwa na faida zaidi kwa watu wengi, sawa ikiwa wako pamoja naye au dhidi yake. Lakini, tukipa upande wa elimu, hakuna nafasi ya kumkosoa mtu huyu kabisa. Isipokuwa yale niliyoyaashiria punde tu, nayo ni usulubu wake mkali. Ama kuhusu kwamba hatendi haki, ni tuhuma mbovu kabisa na hayasemwi isipokuwa na watu wawili: ima ni mtu mjinga ambaye anatakiwa kusoma, au mkengeukaji. Huyu hatuna njia kwake isipokuwa kumuombea kwa Allaah Amuongoze njia iliyonyooka.”

Amesema (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake “Swifat Swalaat-in-Nabiyy”, ukurasa 68, wakati alipokuwa anazungumzia kuhusu al-Ghazzaaliy wa nyuma:

“Wanachuoni na watu waheshimiwa wengi – Allaah Awajaze kheri – wamemraddi. Kwa njia ya ufafanuzi wamebainisha upindaji na upotevu wake. Miongoni mwa Radd bora nilizosoma, ni ile ya rafiki yetu Dr. Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy kwenye gazeti “al-Mujaahid” la kiafghanistani, namba tisa na kumi na moja[2], na yale yaliyoandikwa na ndugu yetu muheshimiwa Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aal ash-Shaykh kwa jina la “al-Mi´yaar li ´Ilm al-Ghazzaaliy”.”

Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) ameandika kama taaliki kwa kitabu cha Shaykh Rabiy´ “al-´Awaaswim mimmaa fiy Kutub Sayyid Qutwub min al-Qawaaswim”:

“Yote uliyomkosoa Sayyid Qutwub ni haki na ni sawa. Hivyo itambainikia kila msomaji Muislamu ambaye angalau ana maarifa kidogo ya Uislamu, ya kwamba Sayyid Qutwub hakuwa na elimu yoyote juu ya Uislamu, si katika misingi yake wala matawi yake. Ee ndugu Rabiy´! Allaah Akujaze kheri kwa kuwa umetimiza wajibu huu wa kufafanua na kufichukua ujinga na upotofu wake kutokamana na Uislamu.”

Mimi mwenyewe nimeona barua hii kwa hati ya mkono wa Shaykh kwenye Maktabah binafsi ya Shaykh, ambayo kwa hivi sasa ipo Maktabah ya Chuo Kikuu cha Kiislamu. Nikachukua kopi yake na ipo nyumbani kwangu.

Shaykh Rabiy´ anachukuliwa ni katika wanafunzi wakubwa na wa kwanza wa Shaykh al-Albaaniy. Shaykh alimfundisha kwenye Chuo Kikuu cha Kiislamu al-Madiynah an-Nabawiyyah.

[1] Katika kipindi cha mwisho Abul-Hasan alidhihirisha njama zake dhidi ya Da´wah ya Salalafiyyah na kupiga vita madhehebu yake na wafuasi wake. Kwa ajili hiyo maneno ya Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) yanamgusa yeye ”Ima ni mjinga au ni mtu anayefuata matamanio yake”. Uhakika wa mambo ni kwamba hiyo ya mwisho iliyotajwa ndio inamgusa. Tunamuomba Allaah kinga kutokana na shari yake na tunamuomba ima Amuongoze au Auvunje mgongo wake.

[2] Kwa anwani ”ad-Difaa´ ´an as-Sunnah wa Ahlihaa”

  • Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
  • Imechapishwa: 28/11/2019