´Aliy al-Halabiy ni katika watu wabaya zaidi wanaoshuhudia batili. Anashuhudia kwa watu wapotevu na wenye misingi ilioharibika na mifumo batili ya kwamba ni Salafiyyuuun, amesimama upande wao na kutumia misingi na mifumo yao. Miongoni mwa watu hawa ni:

2- Muhammad al-Maghraawiy:

Fitina za ´Ar´uur zimefanya Muhammad al-Maghraawiy kutumbukia kwenye Takfiyr za kuweweseka za wendawazimu. Wakati Salafiyyuun walipoonesha makosa yake kutoka kwenye vitabu vyake na mikanda yake akawatuhumu kuwa ni wanafiki.

Wanachuoni wa Salafiyyuun wakapata khabari ya upetukaji mipaka ya Takfiyr ya al-Maghraawiy, wakamnasihi na kumuomba kujirejea ambapo akawatukana, akawapuuza na akawachochea wanafunzi zake kuwashambulia Salafiyyuun ili wapotee zaidi. Ni kana kwamba wanatoka kwenye mduara wa ndani wa Qutbiyyuun na Ikhwaaniyyuun ambao wanampa pesa ili kuwapiga vita Salafiyyah na Salafiyyuun.

Pamoja na kwamba al-Halabiy anaonesha kuwa anapiga vita Takfiyr na Takfiyriyyuun anamlinda na kushuhudia mpaka hii leo ya kwamba al-Maghraawiy ni Salafiy. Je, kitendo chake hichi si mfano wa ushuhudiaji wake wa batili ilio kubwa, mgongano mkubwa na ushirikiano wa kuwaangusha wanachuoni wa Tawhiyd na Sunnah ambao wanapuuzwa na al-Maghraawiy, ´Ar´uur na al-Ma´ribiy? Je, msimamo wake huu hauendi kinyume na mfumo wa Salaf watukufu?

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
  • Imechapishwa: 08/01/2017