29. Sifa na majina ya Allaah yaliyothibiti katika Qur-aan VII

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Amesema (Ta´ala):

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا

”Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?” (04:87)

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا

”Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?” (04:122)

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ

”Na Atakaposema Allaah: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!” (05:116)

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا

”Na limetimia Neno la Mola wako kwa kweli na uadilifu.” (06:115)

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

”Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja kwa moja.” (04:164)

مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ

”Miongoni mwao [yuko] aliyesemeshwa na Allaah.” (02:253)

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ

“Na alipokuja Muwsaa katika pahala pa miadi yetu na Mola wake Akamsemesha.” (07:143)

وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا

”Na Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.” (19:52)

وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰ أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

”Na Mola wako Alipomwita Muwsaa [kumwambia]: “Nenda kwa watu madhalimu.” (26:10)

وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ

 
”Na Mola wao Akawaita [wote wawili na kuwaambia]: “Je, kwani Mimi Sikukukatazeni mti huo.”(07:22)  

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ

 
”Na Siku Atakapowaita na kusema: “Mliwajibu nini Mitume?” (28:65)  

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ

 
”Na ikiwa mmoja wa washirikina akikuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie Maneno ya Allaah.” (09:06)  

وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ

 
”Na hali lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia Maneno ya Allaah kisha wakayapotosha baada ya kuyaelewa na hali wanajua.” (02:75)  
 
 

يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا كَلَامَ اللَّـهِۚ قُل لَّن تَتَّبِعُونَا كَذَٰلِكُمْ قَالَ اللَّـهُ مِن قَبْلُ

 
”Wanataka kubadilisha Maneno ya Allaah. Sema [uwaambie]: “Hamtotufuata! Hivyo ndivyo Alivyosema Allaah kabla”.” (48:15)  

وَاتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَ ۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ

 
”Na soma uliyoletewa Wahy katika Kitabu cha Mola wako. Hakuna awezaye kubadilisha Maneno Yake.” (18:27)  

إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَكْثَرَ الَّذِي هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ

 
”Hakika hii Qur-aan inawasimulia wana wa Israaiyl mengi ambayo wao wanakhitilafiana nayo.” (27:76)  

 

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ

”Na hiki Kitabu Tumekiteremsha kilichobarikiwa.” (06:155)

لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا الْقُرْآنَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ

”Lau Tungeliiteremsha hii Qur-aan juu ya mlima, basi ungeliuona unanyenyekea na wenye kupasukapasuka kutokana na kumuogopa Allaah.” (59:21)

وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ ۙ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ

”Na Tunapobadilisha Aayah mahala pa Aayah nyingine, na Allaah Anajua Anayoyateremsha, [makafiri] husema: “Hakika wewe ni mzushi.” – bali wengi wao hawajui. Sema: Roho Takatifu [Jibriyl] ameiteremsha kutoka kwa Mola wako kwa haki ili Awathibitishie walo walioamini na ni uongofu na bishara kwa Waislamu. Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: “Yuko mtu anayemfundisha. Lugha ya huyo wanaye muelekezea ni ya kigeni na hii ni lugha ya Kiarabu bayana.” (16:101-103)

MAELEZO

Aayah zote hizi tukufu ni zenye kubainisha na kuthibitisha sifa za Allaah (Jalla wa ´Alaa). Kumeshatangulia sehemu ya Aayah. Hizi ni zenye kubainisha maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Allaah alisema, anasema na atasema:

Dalili ya Maneno na Kuzungumza kwa Allaah

وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ

”Na Atakaposema Allaah: “Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam!” (05:116)

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا

”Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?” (04:122)

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا

”Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?” (04:87)

يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا كَلَامَ اللَّـهِ

”Wanataka kubadilisha Maneno ya Allaah.” (48:15)

وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا

”Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja kwa moja.”(04:164)

Aayah kuhusiana na hili ni nyingi zinazothibitisha maneno, wito na kunong´oneza:

وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ

 
”Na Siku Atakayowaita… ” (28:62)  

وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا

”… na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.”(19:52)

Hakika Yeye (Subhaanah) alizungumza na anazungumza pale anapotaka. Aliita na anaita pale anapotaka. Anamzungumzisha amtakaye katika waja Wake kama alivyomzungumzisha Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) na atawazungumzisha walioko Peponi. Vilevile alimzungumzisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku aliyopandishwa. Yote haya yalitokea. Hakika Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) anakijua kila kitu na hakuna kinachofichikana Kwake (Jalla wa ´Alaa).

Qur-aan imeteremshwa na Wahy ukateremka kwa Mitume (´alayhimus-Salaam). Yeye yuko juu (Jalla wa ´Alaa). Ameteremsha Kitabu Chake kutoka juu. Amesema (Ta´ala):

Dalili kwamba Qur-aan imeteremshwa kutoka kwa Allaah

قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ

Sema: Roho Takatifu [Jibriyl] ameiteremsha kutoka kwa Mola wako kwa haki.” (16:102)

Hakika Yeye (Subhaanah) yuko juu. Ameteremsha Vitabu Vyake Tawraat, Injiyl, Qur-aan na Zabuur. Vyote vimeteremshwa kutoka kwa Allaah. Yote haya ni wajibu kumthibitishia Allaah na kwamba ndio maneno ya kweli kabisa kutoka kwa viumbe Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Kadhalika inatakiwa kuamini kwamba Qur-aan ni uongofu kwa watu, kwamba ameiteremsha kwa lugha ya kiarabu na kinawasimulia wana wa Israaiyl mengi ambayo walikuwa wakitofautiana. Yote haya ni haki ambayo ni wajibu kuyaamini na kuamini yale yote yaliyoelezwa na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu maneno Yake, wito Wake, Kauli Yake, uteremshwaji wa Kitabu Chake na Vitabu vya Mitume wengine (´alayhimus-Salaam).

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni wenye kumthibitishia Allaah sifa hizi kwa njia inayolingana na utukufu Wake na kwamba Alisema na Anasema, Alizungumza na Anazungumza, Alinong´ongeza na Ananong´oneza, Alizungumza kwa siri na Anazungumza kwa siri pindi anapotaka na kwa namna anayotaka (Subhaanahu wa Ta´ala).

Allaah anazungumza pale anapotaka

Kuhusiana na maneno ya wanafalsafa ya kwamba maneno ni ya kale ni batili. Alizungumza na anazungumza pale anapotaka. Alimzungumzisha Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) usiku wa Mi´raaj katika wakati wake. Alimzungumzisha Mtume Wake Muusa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) katika wakati wake. Atazungumza na watu siku ya Qiyaamah katika wakati wao. Alizungumza na Aadam (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) katika wakati wake. Atazungumza na watu wa Peponi katika wakati wao. Ni Mwenye kuzungumza (Subhaanahu wa Ta´ala) siku zote pale anapotaka. Kama alivyozungumza hapo kale pia hivi sasa ni Mwenye kuzungumza. Hakuna chenye kumzuia na kufanya hivo (Jalla wa ´Alaa). Anazungumza pale anapotaka. Hutaka pale anapotaka. Huamrisha pale anapotaka. Hukataza pale anapotaka. Hakuna mwenye kumzuia kufanya hivo (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com