170- Mambo matatu yanapelekea kuipa nyongo dunia: kukata mipango katika mustaqbal, kuyafikiria mauti na kuyatembelea makaburi.

171- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuwa katika dunia hii kama mgeni au mpta njia. Jizingatie kama maiti.”[1]

172- Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Usiku ukiingia usitarajie kufika asubuhi na asubuhi ikiingia usitarajie kufika usiku. Tumia fursa ya afya yako kabla ya maradhi na uhai wako kabla ya kufa kwako.”

173- ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitupitia na sisi tuko tunarekebisha kibanda chetu. Akasema: “Hiki ni kitu gani?” Tukasema: “Tuko tunarekebisha kibanda chetu kilichoharibika.” Akasema: “Ninaweza kuona kitu chenye kuja kwa haraka kuliko hicho[2].”[3]

at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

174- Wuhayb bin al-Ward amesema:

“Nuuh (´alayhis-Salaam) alijenga nyumba ya mianzi. Alipoulizwa ni kwa nini hakujenga kwa kitu kingine akasema: “Ni mengi kwa mtu ambaye attakufa.”

175- ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alilala kwenye mkeka kipande. Alipoamka kukawepo athari yake ubavuni mwake. Tukasema: “Ee Mtume wa Allaah! Unasemaje lau tutakuandalia godoro ulale juu yake?” Akasema: “Niko wapi mimi na dunia? Mimi si mwengine isipokuwa ni kama mpanda naegama chini ya mti halafu ninatoka hapo na kuuacha.”[4]

176- Abu Wa´iyl amesema:

“Mu´aawiyah alimtembelea Abu Haashim bin ´Utbah ambaye alikuwa amelala hali ya kuwa ni mgonjwa akamwambia: “Ee mjomba! Ni kwa nini unalia? Ni kwa sababu ya maumivu au ni kwa ajili ya kuipenda dunia hii?” Akajibu: “Si hili wala lile. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichukua ahadi kwetu ambalo hatukulitimiza. Amesem (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mali yote inatosheleza kukusanya mfanya kazi na kipando katika njia ya Allaah.”

Naona nilivyokusanya nyumbani kwangu.”[5]

[1] al-Bukhaariy (6416), at-Tirmidhiy (2333) na Ibn Maajah (4114).

[2] al-´Adhiymaabaadiy amesema:

”Bi maana ninaweza kuona mauti yenye kuja haraka kuliko kibanda hichi.” (´Awn-ul-Ma´buud)

Tazama http://library.islamweb.net/newlibrary/display_book.php?idfrom=9082&idto=9085&bk_no=55&ID=1905

[3] Abu Daawuud (5236), at-Tirmidhiy (2438), Ibn Maajah (4160) na Ahmad (2/161).

[4] at-Tirmidhiy (2483), Ibn Maajah (4109) na Ahmad (1/391).

[5] at-Tirmidhiy (4013).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 106-108
  • Imechapishwa: 18/03/2017