29. Ni nani bora zaidi kati ya hawa wawili?

Swali 29: Maneno ya waliyosema kwamba kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah inazingatiwa ni kupambana katika njia ya Allaah ni sahihi au hayana ukweli wowote?

Jibu: Ndio. Mwenye kupambana na Ahl-ul-Bid´ah ni Mujaahid. Hili ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote. Ahmad bin Hanbal alipoulizwa ni nani bora kati ya ambaye anafunga, anaswali, anatoa swadaqah, anafanya I´tikaaf na mambo ya kheri chungu mzima na mwengine anawaraddi wazushi, akajibu ifuatavyo:

“Ambaye anaswali, anafunga, anatoa swadaqah na anafanya I´tikaaf, haya yote ni mambo yake mwenyewe. Ama ambaye anawaraddi wazushi haya [maslahi yake yanaenea] kwa watu.”

Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote ya kwamba ambaye anawaraddi wazushi ni bora zaidi. Maimamu wana maneno mengi kuhusu hili.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017