Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya nadhiri ni Kauli Yake (Ta´ala):

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا

“Wale ambao wanatimiza nadhiri zao na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea.” (al-Insaan 76 : 07)

MAELEZO

Nadhiri pia ni ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) amesema:

يُوفُونَ بِالنَّذْرِ

“Wale ambao wanatimiza nadhiri zao.” (76:07)

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ

“Chochote mnachotoa au mkiwekacho nadhiri, basi Allaah anakijua.” (02:270)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Aliyetia nadhiri ya kumtii Allaah basi na amtii na aliyetia nadhiri ya kumuasi Allaah asimuasi.”[1]

Nadhiri ni ´ibaadah na ni kumtii Allaah. Mtu mwenye kuweka nadhiri ni lazima aitimize. Hata hivyo imechukizwa kuweka nadhiri kwa kuwa ndani yake kuna malazimisho na uzito. Kwa ajili hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza nadhiri na kusema:

“Nadhiri haileti kheri. Bali inatoka kwa mtu bakhili.”[2]

Lakini mtu akiweka nadhiri ya utiifu basi ni lazima kuitimiza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Aliyetia nadhiri ya kumtii Allaah basi na amtii.”

Mtu akiweka nadhiri ya ´ibaadah kama swalah, swawm au swadaqah, ni lazima aitimize.

[1] al-Bukhaariy (6696).

[2] al-Bukhaariy (6608) na Muslim (1639).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 03/01/2017