29. Mwenye busara na kutangamana na watu II

1- Kila matangamano ambayo mtu hafaidiki nayo basi kukaa na mbwa ni bora. Mwenye kutangamana na mtu muovu hasalimiki kama ambavyo yule ambaye anaingia sehemu ovu anatuhumiwa.

2- al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Kukosa kwako kukubwa ni wewe kumkosa mtu ambaye daima ana kitu cha kukwambia na kukunasihi pale unapomuhitajia zaidi. Unapomkosa basi unamtafuta mwengie pasi na kumpata yeyote.”

3- Wahb amesema:

“Allaah anaweza kuliokoa kabila zima la watu kwa ajili ya mtu mmoja mwema.”

4- Ni wajibu kwa mwenye akili kumtaka ulinzi Allaah kutokamana na kusuhubiana na matangamano maovu ambao hawamsaidii pale anapomdhukuru Allaah (Ta´ala) na ambao hawamkumbushi pale anapomsahau na pale anapoghafilika wanamshaji´isha kutokukumbuka.

5- Yule ambaye yuko na marafiki waovu basi yeye ndiye muovu wao zaidi. Kama ambavyo mtu mwema hasuhubiani isipokuwa na watu wema basi vivyo hivyo muovu hatangamani isipokuwa na watenda madhambi. Mtu akilazimika kukaa na mtu basi akae na watu walio na muruwa.

6- ´Abdul-Waahid bin Zayd amesema:

“Kaa na watu wenye dini katika watu wa dunia na usikae na watu wengine. Endapo utalazimika kukaa na mtu basi kaa na watu wenye muruwa. Kwani wao hawana upuuzi katika vikao vyao.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 101-103
  • Imechapishwa: 16/02/2018